GET /api/v0.1/hansard/entries/1219562/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219562,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219562/?format=api",
"text_counter": 184,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono Taarifa iliyoletwa na Sen. Faki kuhusu ukakatwa kwa umeme katika hospitali ya Mombasa. Bw. Spika, swali langu ni hili: Je, wagonjwa wanalipa wanapoenda kutibiwa katika hospitali hii ya Mombasa? Kama hawalipi, jibu la swali langu litakuwa tofauti. Hospitali hizi zetu tunazojadili hapa, mtu akifariki hupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Watu wanapoenda kuchukua mwili, hulipa kiwango fulani cha pesa. Ikiwa wagonjwa hulipa wanapotibiwa na miili inapochukuliwa kutoka chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali hii, pesa hizo huenda wapi?"
}