GET /api/v0.1/hansard/entries/1219564/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219564,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219564/?format=api",
    "text_counter": 186,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Nimemsikiliza Sen. Thang’wa akisema kuna hela zinatengwa na Seneti za hospitali za kaunti zote nchini. Kuna pesa za Mombasa, Laikipia na kaunti zingine. Pesa hizi huwa zinaenda wapi? Ninakashifu ule ukataji wa nguvu za umeme na Kampuni ya Nguvu za Umeme Nchini. Bw. Spika, tujiulize maswali ambayo ni mazito. Wale ambao wanaohusika na msimamizi wa hospitali zetu, kwa nini hawalipi deni au bili ya stima? Ningependa Mwenyekiti aulize kama kulikuwa na notisi na ya siku ngapi kabla ya kukata stima katika hospitali hiyo kwa ajili ya wale wagonjwa walio katika vyumba vya wagonjwa mahututi. Je, kuna maadishi kuhusu notisi iliyotolewa? Waswahili husema, mgala muue na haki umpe. Leo tutasema stima zisikatwe mahospitalini. Kesho tutasema stima isikatwe katika vituo vya polisi kama vile alivyosema Seneta mwenzangu. Bw. Spika, Seneti imetenga pesa ambazo zinazoenda katika kaunti zetu. Sisi kama maseneta tunazembea kazini ikiwa hatutahakikisha kuwa walimu wetu wa chekechea wanalipwa mishahara yao, Kampuni ya Nguvu za Umeme Nchini inalipwa madeni yake na huduma nyingine kufanyiwa wananchi. Nampongeza Sen. Faki kwa kuleta Taarifa hii. Inafaa iwe funzo kwa kaunti zetu zingine ndio magavana wajue wana jukumu la kuhakikisha kila deni limelipwa. Bw. Spika, ulikuwa gavana wa Kaunti ya Kilifi na unajua vile mgao wa fedha kutoka Serikali Kuu hucheleweshwa. Mashirika ya Serikali yanafaa kujadiliana na hospitali zetu badala ya kukata stima bila notisi. Nakemea Kampuni ya Nguvu za Umeme Nchini sababu huwa na mbio kukata stima ya yule ambaye hajalipa. Hata hivyo, ukitembea nyumba zetu, vyakula vinaoza sababu stima hupotea kila mara. Juzi, Kenya nzima kulikuwa na giza. Hakuna mtu yeyote aliyepata fidia kutoka kwa kampuni hii. Mimi nilikuwa nimelipa deni yangu ya stima yangu. Kwa hiyo, haikuwa makosa yangu ila ya kampuni. Jokovu langu au kifaa chochote kikiharibika sababu ya nguvu za umeme kupotea, nina haki kulipwa fidia sababu hiyo si shida yangu bali ni ya kampuni ya umeme. Jambo hili tutalifuatilia mpaka vitongojini ndio tuone ya kwamba tumepata suluhu la kuhudumu. Tukinyamaza na kusema ni watu wa Pwani wanaangamia, kampuni hii itakakata stima Kilifi, Makueni, Nairobi na kaunti zote nchini. Watakapofika Laikipia, hakuna mtu yeyote atakuwepo kusema Laikipia tunamalizwa. Ninaunga mkono."
}