GET /api/v0.1/hansard/entries/1219566/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219566,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219566/?format=api",
"text_counter": 188,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa hii fursa umenipa ili kuunga mkono Taarifa ya Seneta wa Mombasa, Sen. Faki, kuhusu kitendo cha Kampuni ya Nguvu za Umeme Nchini cha kukata stima katika hospitali ya Rufaa ya Mombasa. Ninakikashifu kitendo hicho kwa kinywa kipana kwa sababu ni cha kufa na kupona. Suala la kukata stima katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Pwani, ni la kutamausha, kuhuzunisha na ni lazima tulikashifu vilivyo. Wale walio katika ile hospitali ni wake, waume au watoto wetu. Mtoto wako akiwa katika ile hospitali, akifa unaweza kuzaa mwingine, lakini yule tayari ashakufa."
}