GET /api/v0.1/hansard/entries/1219588/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219588,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219588/?format=api",
"text_counter": 210,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Bw. Spika, hata kama mama yako ataolewa na mume mwingine na upate baba mwingine, yule mzee ashakufa tayari. Ningependa kujihusisha na matamshi ya Sen. Mandago ya kwamba jambo hili lilitokea kwa sababu ya ukiritimba wa kampuni hii ya umeme. Inafaa tulete Mswada katika Bunge hili ya kuwapa watu wengine haki ya kusambaza umeme. Hili tendo la kampuni hii ni kwa sababu ya ukiritimba; kwamba ni wao peke yao ambao wanasambaza umeme. Kungekuwa na mashirika mengine ambayo wanashindana nao labda hilo tendo halingetokea. Kwa upande mwingine ni lazima tujiulize swali hili. Je, Serikali ya Kaunti ya Mombasa imejizatiti namna gani kuhakikisha madeni ya kampuni hii yamelipwa? Ndio maana ninasema ya kwamba hii Taarifa ikipelekwa kwa Kamati ya Afya, ni lazima wadau wote waje, wakiwemo wakurugenzi wa kampuni ya umeme na viongozi wa Kaunti ya Mombasa. Waje watueleze ni kwa nini stima inaweza kukatwa katika taasisi muhimu kama hospitali."
}