GET /api/v0.1/hansard/entries/1219611/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219611,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219611/?format=api",
"text_counter": 233,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13733,
"legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
"slug": "agnes-kavindu-muthama"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa hii ambayo imeletwa na Seneta wa Kaunti ya Mombasa. Bw. Spika wa Muda, ni tabia mbaya sana kwa kampuni ya umeme kukata stima katika hospitali za kaunti. Ninakumbuka kwamba katika Kaunti ya Machakos, mwaka uliopita, umeme ulikatwa ilhali kulikuwa na wagonjwa waliokuwa kwa oxygen . Nilipigiwa simu nikaambiwa niende huko hospitalini kwani kulikuwa kumeharibika baada ya stima kukatwa kwa muda wa siku mbili. Mama yule aliaga dunia mara tu nilipofika Kaunti ya Machakos. Kabla sijafika hospitalini, nilimpigia County ExecutiveCommittee Member (CECM) wa Kawi katika Kaunti ya Machakos. Nilimuamurisha kwamba nikifika hapo, nipate stima imewaka hospitalini. Hakika, stima hiyo ilikuwa imekatwa maksudi. Nilipata wamewakisha stima. Hospitali ililipa deni yao na stima ikarudishwa. Kabla hao watu wa kampuni hii hawajakata umeme, ni vizuri wawe wakiwasiliana na mazimamishi wa kaunti na kuwapa fursa ya kulipa deni ya umeme. Ni kweli kuwa kampuni hii ya umeme haitaendelea kusambaza umeme tu bila malipo lakini ni makosa sana kwao kukata umeme kwa hospitali. Magavana wengine hawaajibiki kulipa deni au bili za stima za hospitali za kaunti zao ili watu wetu wanaendelea kuumia bure katika hospitalini zetu. Sen. Faki, ninakushukuru kwa kuleta hii Taarifa hii . Niko katika harakati za kuchukua rekodi ya watoto na watu wazima walioaga katika hospitali ya Machakos wakati kampuni hii ya umeme ilikataa stima. Nitaleta Taarifa hapa kwa maana hao watu lazima wafidiwe na kampuni ya umeme. Ni lazima walipwe. Sen. Faki, Seneta wa Kaunti ya Mombosa nakusihi ufanye uchunguzi na kubaini ikiwa maafa yoyote yalitokana na kukatwa kwa huo umeme katika hospitali hiyo ya Mombasa. Ikiwa kuna watu walikufa, lazima walipwe. Ni lazima watoto waliokuwa kwenye incubator waliaga, watu waliokuwa katika kitengo cha Intensive Care Unit (ICU), waliokuwa wanafanyiwa dialysis na wale ambao walikuwa kwa oxygen, lazima waliteseka na wegine kuaga dunia. Watu hao lazima walipwe. Kenya Power na magavana lazima waajibike. Ninaomba Sen. Faki unisikilize maana ni wewe umeleta Taarifa hii hapa Seneti. Lazima ufuatilie suala hili kwa kina katika Kaunti ya Mombasa. Pia mimi naahidi kuchunguza suala hili katika Kaunti ya Machakos. Naomba pia maseneta wengine wafuatilie suala hili katika kaunti zao. Sen. Faki, ni lazima ufuatilie ujue ni watoto wangapi wakifa kutokana na kukatwa kwa umeme; wale walikuwa kwenye incubator, kwenye oxygen, kwa ICU na wale walikuwa wanafanyiwa dialysis ili ulete hiyo hesabu vizuri hapa tunapoendelea na huu mjadala. Kamati itakapowaalika hapa Seneti wahusika wote ni sharti uwe na hesabu kamili. Pia mimi nitaleta hesabu ya watu wote walioathirika katika Kaunti ya Machakos. Bw. Spika wa Muda, ninaomba watu wote waliohusika, wachukuliwe hatua kali na ile kamati ambayo kauli hii itakabidhiwa itinde haki. Naomba kaunti zote kuzingatia umeme wa solar panels kwa hospitali. Hospitali zingine hazina hata generator as a backup. Stima ikienda, generator inafaa kuwaka"
}