GET /api/v0.1/hansard/entries/1219621/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219621,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219621/?format=api",
"text_counter": 243,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cherarkey",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13217,
"legal_name": "Cherarkey K Samson",
"slug": "cherarkey-k-samson"
},
"content": "kwa kuleta Taarifa muhimu. Nilishangaa nilipoona kwenye vyombo ya habari kampuni ya umeme imezima umeme kwa sababu ya mambo kadha wa kadha. Umeme ni muhimu sana. Ningependa Bunge la Seneti au Kamati husika ihakikishe imetoa makataa kwa kampuni ya umeme. Ikiwa kunaye aliaga dunia kwa sababu ya ukosefu wa umeme katika Hospitali Kuu ya Mombasa mhusika anafaa kuchukuliwa hatua ya kisheria. Mambo kama haya yanaharibu uchumi. Hii ni economicand health sabotage. Hili ni swala la haki za kibinadamu. Kuna watoto waliotegemea umeme huo na pia madawa yalikuwa yanategemea jokofu ili yatumike kwa muda fulani. Kwa hivyo, hii ni hasara kubwa. Ninauliza kampuni ya umeme katika taifa hili la Kenya iwasiliane na hospitali zetu wanapokata umeme na washirikiane na wasimamizi wa hospitali zile ili tusipoteze maisha. Nafikiri kampuni ya umeme imepitia changamoto nyingi. Mvua inapokaribia kila wakati umeme unapotea. Tunapata malalamishi ya transformers ambazo hazifanyi kazi nchini. Vile vile, hakuna metres ambazo wanawekea wananchi kutoka kaunti za Garissa, Mombasa au Nandi kuwezesha nguvu za umeme kuwafikia. Kuna shida kubwa katika usimamzi wa kampuni ya umeme. Ninaomba Seneti na Kamati husika iwachukulie hatua kali za kisheria na wazipe ridhaa familia ambazo zimepoteza watu wao. Katika Taarifa hii ya ndugu yetu, ameongeza kuwa kuna utepetevu wa wafanyikazi wa hospitali hio. Kaunti ya Mombasa inayoongozwa na gavana inafaa kuchukuliwa hatua kali. Kwa sababu hakufai kuwa na utepetevu katika utoaji wa huduma za afya hospitalini ya Coast General Hospital ambayo ni hospitali kubwa ya rufaa inayohudumia kaunti nyingi katika sehemu za Pwani. Kwa hivyo, wanafaa kuchukuliwa hatua ili malalamishi haya yakome. Maswala ya afya ni devolved function ambayo iko kwa Ratiba ya Nne ya Katiba. Kama kaunti zitashindwa kusimamia maswala ya afya katika taifa la Kenya, itakuwa ni kosa kubwa sana. Ninaunga mkono na kumshukuru, Sen. Faki. Ikiwezekana, Kamati husika ya maswala ya Afya inafaa kuzuru Kaunti ya Mombasa ili tujue hali ilivyo mbashara. Wanasema vitu kwa ground ni tofauti. Kwa hivyo, inabidi Kamati iingilie kati na kushugulikia mambo haya. Bw. Spika wa Muda, ninashukuru kwa kunipa fursa hii. Ninampa kongole na heko, Sen. Faki."
}