GET /api/v0.1/hansard/entries/1219627/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219627,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219627/?format=api",
"text_counter": 249,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Nilikuwa nimeketi hapa kama nimetulia tuli nikisikiza na nikaona sura ambazo nazijua. Wamenyonga tai na mabinti wamekula vyema na nyuso zao nyororo kama watu wa Kaunti ya Bungoma. Ninashukuru sana kuja kwao hapa kwa sababu ugatuzi kuafiki malengo yake ni lazima viongozi katika Bunge la Kaunti la Bungoma na kaunti nzima wajue kuifanya kazi yao na majukumu yanayoambatana na matarajio ya wananchi. Pia, wajumbe wa ward wanapochangia pale mashinani, viongozi hawa ndio huhakikisha maoni na maelezo ya viongozi yanawekwa kwenye vitabu inavyotakikana. Najivunia uchapa kazi wao. Nimekuwa kule vijijini kwa muda mrefu nikifanya kazi na aliyekuwa Seneta wa Kaunti ya Bungoma. Tulikuwa tunazuru Bunge la Kaunti akiwahudumia au kutoa hotuba za mwaka baada ya mwaka. Huu ni wakati wangu kuwakaribisha katika Bunge la Seneti na kuhakikisha kupitia, Bw. Spika, na uwezo niliopewa kikatiba na wananchi wa Bungoma kutembea na nyinyi aste kuhakikisha kuwa mnatimiza majukumu yenu pasipo tisho, ubaguzi, au bugdha yeyote. Ninawakaribisha katika Bunge la Seneti mmejionea kwa macho yenu kwamba mambo yanafanywa sawasawa. Nitatembea na nyinyi kule nyumbani kuhakikisha kwamba shilingi ya mtozwa ushuru wa Bungoma inafanya kazi. Kupitia Spika wenu, Bw. Situma, mchapakazi mwenzangu, ninajua mko mikononi ya mtu mungwana ambaye si mbadhirifu kama kupe lakini mtu wa moyo mweupe kama pamba. Karibuni sana watu wangu wa Bungoma. Najivunia nyinyi kuwa hapa. Mungu awabarikie na mjihisi mko katika Bunge ya viongozi ambao wanatajriba ya kisiasa na taaluma mbalimbali ambapo sheria zinatungwa vizuri. Asante kwa kunitunuku nafasi hii ya kuwakumbatia kupitia kipaza sauti watu wangu wa Kaunti ya Bungoma. Asanteni na Mungu awabariki."
}