GET /api/v0.1/hansard/entries/1219637/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219637,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219637/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "` Sen. Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "hadi Jumatatu yamefanya nikaanza kuwaonea MCA huruma kwa sababu watu walikuwa wanakuja kwangu wakiwa wengi na mimi ni Seneta. Niliona ya kwamba katika kila kijiji mtoto akigonjeka lazima MCA akuwe hapo kumhudumia. Katika mambo ya kanisa, MCA yuko hapo. Ni jambo ya ajabu. Ni aibu kubwa sana kwa sababu hata Seneta wengi hawajawahi kwenda kusema asante kwa kanisa na MCAs wamepanga laini. Kama Embu County, wako 30 MCAs na kila wiki wanaenda kusema asante kwa kanisa. MCA mwenyewe yuko na mambo ya matanga, karo, na kila kitu na unaona ule mshahara anaoupata. Kwa hivyo, Seneti ni vizuri tukae chini tutee MCAs waweze kupata hela nyingi kwa sababu ya ile kazi wanafanya kule mashinani. Pia MCA ndiye anafanya kazi kubwa kuangalia vile gavana anafanya kazi. MCAs huangalia kila kitu, wanapigana kule hata saa ingine wanaambiwa wamekula pesa. Kwa hivyo, mimi niko katika mrengo ya kuunga mkono MCAs waweze kusaidiwa na mambo ya pesa kwa sababu, wanafanya kazi kona zote za kaunti. Kwa hivyo, ningependa kuwapongeza MCAs wote nchini Kenya. Ninaomba Mungu awasaidie mpate hela nyingi. Asante."
}