GET /api/v0.1/hansard/entries/1219639/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219639,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219639/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Kwa hoja ya nidhamu, Bw. Spika wa Muda. Watu wana mbwembwe kuzungumzia mambo ya wajumbe wa wadi. Lakini vijana ambao wako mbele yangu ni wachapa kazi wa Bunge la Kaunti ya Bungoma. Ijapokuwa tunawatetea MCAs wetu ambao wanatekeleza wajibu ambao unastahili kupewa shukrani, lakini hawa wachapa kazi lazima mambo yao vile vile yaangaziwe katika maeneo yao ya kazi. Kwa mfano, lazima wapandishwe madaraja baada ya muda; wapewe nafasi ya kuendesha magari ya kifahari; wapewe nafasi ya kupata matibabu katika hospitali na gharama mbali mbali. Nadhani hawa watu lazima pia mambo yao yaangaliwe. Ama namna gani? Sasa tuko hapo na nyinyi tuhakikishe kwamba MCAs wanapojivunia kuwa MCAs, wachapa kazi katika mabunge 47 nchini Kenya, wao vile vile waweze kupata matunda ya jasho lao na tuongeze pesa katika mabunge haya ili wasimamizi wa Mabunge haya, wapatie vijana wetu nafasi ya kupandishwa mishahara na kujivunia na safari mbalimbali; kufanya utafiti mbalimbali, ili pia wengine wakiomba kazi katika Bunge la Kitaifa mimi nitakuwa tayari kuwashika mkono wakuje hapa wang’are kama hawa wetu wa Seneti na wachape kazi na tujivunie kwamba Bungoma iko na wachapa kazi. Asante sana, Bw. Spika wa Muda."
}