GET /api/v0.1/hansard/entries/1219699/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219699,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219699/?format=api",
    "text_counter": 50,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": " Kwa hivyo, Mhe. Spika, nikiangalia hali ilivyo, lazima kuwe na uongozi mzuri. Ukiangalia bei ya chakula, utagundua hali ni mbaya sana katika nchi wakati huu. Kule Galana Kulalu, Waisraeli walikuja kutusaidia kukuza mazao. Ajabu ni kwamba walifanyiwa finyange nyingi sana mpaka mwishowe wakaondoka humu nchini. Niko na imani kwamba kuna wawekezaji ama wafanyibiashara humu nchini ambao wamejitolea na wanataka kufanya kazi hiyo ya ukuzaji wa chakula pale Galana Kulalu. Jambo kubwa ambalo naliomba ni kuwa Serikali iwaunge mkono ndiposa waweze kufanya kazi vyema. Tukifanya hivyo, matatizo haya yatatuondokea. Kuhusu ombi la pili, tukiangalia hasa kule Mombasa ninakotoka, watoto wengi sana walikuwa wanapotea eti kwa sababu walichukuliwa kuwa Al Shabaab . Hakuna sababu yoyote iliyotajwa ya kuwatuhumu hao vijana. Itakuwaje Serikali inashika kijana na baada ya siku mbili ama tatu hapatikani? Kwa hivyo, ni lazima Serikali ilinde watu wake na kuwe na ubinadamu katika kuwashughulikia. Ikiwa kuna jambo lolote, mtu asipotezwe bali achukuliwe hatua kulingana na ushahidi uliopo. Kwa hayo, Mhe. Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi."
}