GET /api/v0.1/hansard/entries/1219709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219709,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219709/?format=api",
"text_counter": 60,
"type": "speech",
"speaker_name": "Gilgil, UDA",
"speaker_title": "Hon. Martha Wangari",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika. Hata mimi natoa maoni kuhusu dua hili lililowasilishwa Bungeni na Mkurugenzi kutoka Kituo cha Sheria kuhusu kutoweka kwa lazima kwa binadamu. Haya maneno ni ya Katiba. Ni haki za binadamu. Nafikiri jamii nyingi zimeumia sana. Ukiliangalia kijinsia, wale ambao wanatoweka mara nyingi ni wanaume. Watoto wanabaki mayatima na wanawake wanabaki wajane. Tunaomba Kamati hii iangalie mambo haya. Unaweza poteza binadamu lakini afadhali hata upate mwili. Tumefika mahali familia zinaomba zipate tu miili, waizike na wasahau. Mwaka wa 2021, kuna wakili kutoka kijiji kinaitwa Miti Mingi kule Gilgil ambaye alitoweka na hadi leo hatujui yuko wapi. Watoto na wazazi wake wanahangaika. Kwa hivyo, tunatumaini Wanakamati wataleta ripoti hiyo ya mambo haya kwenye Bunge hili ndiyo tuweze kuhakikisha kwamba mambo ya kutoweka ni jinai. Sharti hatua zichukuliwe kama inavyofaa. Asante, Mhe. Spika."
}