GET /api/v0.1/hansard/entries/1219711/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219711,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219711/?format=api",
    "text_counter": 62,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia ombi lililotumwa kuhusu watu kupotea kiholela. Sisi, katika Lamu Kaunti, tumeathirika sana. Tukitaja watu wetu waliopotea na hatujui wako wapi mpaka sasa, orodha ni ndefu. Tulifikiria ni masuala ya Al Shabaab kwa vile tuko mpakani lakini la kusikitisha na kuchanganya watu zaidi ni kuwa hivi karibuni tuliambiwa mauaji ya Lamu Kaunti hayahusiani na Al Shabaab bali ni mambo ya mashamba. Watu ninaowasimamia sasa wanatatizika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}