GET /api/v0.1/hansard/entries/1219712/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219712,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219712/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Hawajui wanaowaua ni nani? Kwa nini watu wetu wakimbie na wateswe kwa sababu ya AlShabaab na kumbe kuna kiongozi anayejua wanavyouawa? Nimefurahia hili ombi. Hata mimi itabidi niifanye iwe kauli au dua ili Serikali ituambie ni nani anawaua watu Lamu. Hilo ni jambo ambalo limetatiza watu sana. Siku nyingi tumekuwa tukifikiri ni Al Shabaab kumbe siyo wao bali ni mambo ya ardhi. Aliyoyasema Kiongozi wa Wengi Bungeni, inamaanisha anawajua wanaowaua watu huko Lamu Kaunti. Na itakuwa vizuri kuwataja kwa sababu imetutatiza sana. Kule, tunategemea utalii. Watalii sasa hawakuji maana kuna askari wengi na msafara wa magari mengi. Wakikuja kama watalii na waone wanajeshi wengi, huwa wanashangaa wanaenda wapi. Hiyo, inawaogofya na wanarudia njiani. Pesa nyingi za Serikali zimekuwa zikitumika katika Operesheni Linda Boni tukijua wanapambana na Al Shabaab . Ingawa hivyo, watu wanapotea ovyo ovyo. Na kwa vile sasa tumejua siyo wao bali ni tatizo la ardhi, tunataka Serikali ijitokeze wazi kuchunguza wanaowaua watu ili uchumi uweze kuendelea katika Lamu Kauti. Asante Bw. Spika."
}