GET /api/v0.1/hansard/entries/1219782/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219782,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219782/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": null,
"content": "Naomba Kutoa arifa ya hoja kuhusu kutekelezwa kwa sheria za kupigwa marufuku mahusiano ya jinsia moja nchini Kenya: KWAMBA, tukifahamu kuwa familia ndio kiungo cha msingi wa jamii, na kutambua kwamba utamaduni wa Kiafrika unathamini sana asasi ya ndoa ambayo inahakikisha kuendelea kwa binadamu kupitia uzazi; tukizingatia ukweli kwamba Ibara ya 45(2) ya Katiba inaeleza kuwa kila mtu mzima ana haki ya kufunga ndoa na mtu wa jinsia tofauti kwa msingi wa hiari baina ya wahusika; tukitambua pia kwamba Kifungu cha 162 cha Kanuni ya Adhabu kinamtia hatiani yeyote ambaye anashiriki tendo la ngono lisilo la kawaida na mtu yeyote kinyume na utaratibu wa asili; tukizingatia kuwa mahusiano na ndoa za jinsia moja na ngono inayotokana na mahusiano haya ni kinyume na utaratibu wa asili; tukisikitika kwamba kumekuwa na ongezeko la mahusiano ya jinsia moja nchini Kenya kutokana na usambazaji wa vitabu na machapisho yanayokuza upotovu huo; tukitambua kwamba uchapishaji na usambazaji wa nyenzo zinazohusu mahusiano ya jinsia moja katika machapisho na vyombo vya habari una athari kali kwa maadili ya jamii kuhusu mwelekeo wa kijinsia; tukimaizi kwamba kuna haja ya kutekeleza sheria ili kulinda na kuhifadhi maadili ya mahusiano ya jinsia tofauti katika taifa; tukifahamu kwamba hakuna uwezekano wa kuzaa kutokana na mahusiano na ndoa za jinsia moja; tukihofia kwamba kuongezeka kwa mahusiano na ndoa za jinsia moja kunaitia jamii ya wanadamu nchini katika hatari ya kutoweka; Bunge hili, hivyo basi, linaazimia kwamba Serikali ipige marufuku mara moja uzungumziaji, uchapishaji na usambazaji wa taarifa zinazokuza mahusiano ya jinsia moja nchini na kuweka mikakati ya kudhibiti maudhui hayo kwa mujibu wa Ibara ya 45(2) ya Katiba na Kifungu cha 162 cha Sheria ya Adhabu ili kuikinga jamii, hasa watoto na vijana, dhidi ya kufikiwa na mielekeo potovu ya mapenzi na ndoa ya jinsia moja yaani ushoga na usagaji almaarufu kwa lugha ya Kiingereza gayism and lesbianism . Shukran sana, Mhe. Spika."
}