GET /api/v0.1/hansard/entries/1219902/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219902,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219902/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinangop, PAA",
"speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
"speaker": null,
"content": " Mheshimiwa Spika wa Muda, ninaomba niiunge Hoja hii mia-fil-mia. Asante sana kwa sababu ya hiyo. Nashukuru sana kupata nafasi hii kwa sababu Hoja hii inajaribu kuleta tiba kati ya maswala mengi ambayo yamekuwa mazito sana katika nchi hii. Tukiangalia tangu mambo ya ugatuzi yalipoingia, maswala ya Kiongozi ya Wachache Bungeni yamekuwa ofisi ambayo haijakuwa na mwakilishi vilivyo; mwakilishi ambaye anahakikisha kwamba maswala yote yanayofanyika kuhusiana na kazi ya Serikali yana mtu anayejaribu kuangazia na kuhakikisha kwamba kazi njema inafanyika katika Serikali hii. Kama Hoja hii itakubalika, ni matumaini yangu kuwa italeta usawa mwingi na kuhakikisha kwamba kazi nyingi zinafanyika Bungeni. Itahakikisha kwamba tunajua tunaelekea wapi wakati Kiongozi wa Wengi na wa Upinzani wanakutana hapa."
}