GET /api/v0.1/hansard/entries/1219903/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219903,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219903/?format=api",
    "text_counter": 254,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kinangop, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
    "speaker": null,
    "content": "Pili, ninafikiri maswala ya NG-CDF kujumuishwa katika Katiba kwa kutaka kuikarabati yanatakikana kupewa kipaumbele. Ndio maana Rais wa jamhuri akatoa taarifa ama maombi yake katika Bunge hili, kwamba Wabunge walijadili. Kutoka kubuniwa kwake, swala la NG-CDF limewapa watu wachache kazi, hasa mahakama na watu wengine tofauti tofauti kukimbia kortini na kuona lengo la kutaka kusambaratisha mradi huu wa NG-CDF. Ninafikiri mahakama ina kazi nyingi muhimu za kufanya. Hata juzi, twashangaa mahakama ilikuwa inazungumzia maswala ya mashoga na wasagaji. Hapa, maswala ya NG-CDF ambayo yangekuwa ya maana sana yanapewa hali tusiyoelewa tunaelekea wapi. Mahakama ina kazi yake huku inafanya ukarabati ambao ungefanywa Bungeni. Kazi hii imeanza kutengenezwa mahakamani. Ndio maana tunasema kwamba pengine ni muhimu sisi wenye kujumuika na maswala kama haya, tujaribu kupata tatuzi ya kuhakikisha kwamba Katiba imefanyiwa ukarabati ili tuhakikishe kwamba sheria hizi zimerekebishwa na kuhakikisha kwamba NG- CDF itakuwa ni kitengo ambacho kinatoa huduma zilizo njema. Tukiangalia jamii zetu kule nyuma, ikifika wakati wa kufunguliwa kwa shule, bursary inapokosekana inakuwa vigumu kwa Mjumbe kwa sababu yeye ndiye anakuwa ATM na hawezi kuyatosheleza maswala haya. Kwa hivyo, ninaomba kwamba kwa wale ambao pengine wangekuwa na roho mbili mbili kuhusu swala hili, wafikirie mara mbili. Hazina ya NG-CDF ni msaada kwa wananchi walio wengi na ni msaada kwa taifa nzima. Kwa sababu katika sehemu mbalimbali miundomsingi inayotengenezwa kwenye shule zetu nyingi inatokana na NG-CDF. Nilipoanza kazi Bungeni mwaka wa 1992 nilikuwa na shule za upili sita peke yake. Kufikia hivi sasa, niko na shule 27 The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}