GET /api/v0.1/hansard/entries/1219904/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219904,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219904/?format=api",
"text_counter": 255,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinangop, PAA",
"speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
"speaker": null,
"content": "na ninashukuru kwamba hizi shule zote ziliweza kupatikana kwa sababu ya hazina ya NG- CDF. Mhe. Spika wa Muda, maswala haya ya jinsia pia yamekuwa ya utata sana kwa zaidi ya karibu vipindi vitatu vya Bunge. Iko haja ya kuhakikisha kwamba jinsia zina uwakilishaji sawa katika Jumba hili. Tumekuwa kila tukijaribu kupiga hesabu zetu mambo hayaendi vile yanavyotakikana na upinzani unakuwa kati yetu sisi wenyewe kwa wenyewe. Upande wa wanaume na upande wa akina mama tunabishana na mara nyingi hatupati suluhisho kiwango kwamba ilifika mahali Jaji Mkuu alitoa ilani kwamba Bunge linaweza likakatizwa kutokana na kucheleweshwa kwa kubuniwa kwa sheria hii. Nina imani kwamba Katiba itakapokuwa imefanyiwa ukarabati na mambo haya yote kujaribu kuangaziwa, hili swala litakuwa historia kwa sababu kila jinsia itajipata ina uwakilishaji tosha ili kuhakikisha kwamba watu wote wanapata uwakilishi vilivyo. Swala la Mawaziri kuingia katika hili Bunge litakuwa la manufaa sana kwetu kwa sababu wakati mwingine inatakikana tuangalie sheria vile ilivyo. Sheria ilitengenezwa na mwanadamu na inaweza kukarabatiwa na mwanadamu na mahali ambapo tunaweza tukatumika ili kuhakikisha kwamba ukarabati umefanywa, ninaona ni bora tuhakikishe kwamba sheria hii inafanyiwa ukarabati ili Mawaziri wapate kuja Bungeni. Tumewahi kuwa na visa vingi ambavyo vinahitaji Mawaziri kufika katika Bunge hili ili kueleza kinagaubaga kinachoendelea katika wizara zao. Lakini wakati mwingi tunapotegemea kamati huwa nazo pia zinategemea kupata majibu kutoka kwa wizara, na wakati mwingine wanashindwa kutupa majibu. Mara nyingi watu wameleta petition hapa na kuuliza s tatement lakini majibu wanayoyapata kutoka kwa kamati wakati mwingine yanashida kuchambuliwa vilivyo kwa sababu majibu hayako sahihi na hayawezi kutusaidia. Sasa inakuwa ni kama ambao tunauliza petitions zile, maswala yale lakini hakuna mtu ambaye yuko tayari kusema ule ukweli jinsi ulivyo. Nina imani kwamba hawa Mawaziri watakapoanza kutumika hapa, maswala mengi ambayo yamekumba nchi hii, kama yale tulikuwa tukizungumzia mchana wa leo kuhusiana na usalama wa nchi hii, mengi yatapata kuwa na mwisho. Ninakumbuka wakati fulani mwaka jana watu wangu wa Mwembeni walivamiwa na watu arobaini walio na silaha katika boma na kituo cha polisi ni kama kilomita tano. Lakini kwa sababu inaonekana kwamba watu wa usalama walikuwa wamehusika kuhakikisha kwamba watu wale watatekeleza ujangili ule, hawakuweza kujihusisha vilivyo. Hata baada ya kituo cha polisi cha mbali kilipofika, magari yaliyonaswa na watu fulani kushikwa, kilicho tushangaza ni kwamba baada ya watu hawa kupelekwa mahakamani, wakili wa Serikali alikuja mahakamani akasema kwamba anaisitisha kesi pasipokuwa na sababu. Ushahidi umepatikana. Ushahidi ulikuwa, magari na watu wameshikwa, lakini wakili wa Serikali akasitisha kesi. Ni jambo la kusikitisha kwamba kutokea wakati huo mpaka sasa, hatujakuwa na suluhisho ya kujua watu ambao nyumba zao zilichomwa na wakapigwa, haswa akina mama na watu wazima hatima yao imebaki wapi. Kama ilikuwa pengine ni njia ya kuwahamisha, utaratibu haukufuatwa na sheria ilivunjwa. Kwa nini mpaka sasa hakujachukuliwa hatua yoyote ya kuhakikisha kwamba usalama umepatikana? Tukiuliza statement, tunapata majibu ambayo hayaeleweki na Mawaziri hawapatikani kwa sababu sheria inawakataza kufika Bungeni. Kwa hivyo, Mhe. Spika wa Muda, ninakubali na kuiunga mkono Hoja hili, nikiamini kwamba kiongozi wa nchi aliona kwamba ni vyema Bunge likapate kujumuika vilivyo kwa sababu ni kati ya majukumu yetu kuhakikisha kwamba ukarabati umefanywa na mambo haya yameingizwa kwenye Katiba ili tupate huduma zilizo bora. Ninashukuru kwamba kufikia wakati huu tumeanza kupata pesa kidogo za NG-CDF lakini vile zinavyokuja, hata wakati mwingine inabidi kamati ya NG-CDF, mwenyekiti ama Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi, kulazimika kutoa majibu ambayo hayaeleweki kwa sababu Waziri wa Fedha hajafika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}