GET /api/v0.1/hansard/entries/1219912/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219912,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219912/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii niweze kuchangia Hoja hii inaelekeza kurekebisha Katiba. Kwanza, ubunifu wa ofisi ya mkuu wa upinzani katika Katiba itatupunguzia maswala ya vurugu katika nchi mara kwa mara baada ya uchaguzi. Vile vile, tunapofikiria ofisi za Wawakilishi wa Kike wa Kaunti zipate mgao ili kina mama waweze kusaidia makundi yao, tunaendelea vizuri. Katika swala la pesa za NG-CDF, msemaji mwenzangu ameongea vizuri lakini nataka nimufahamishe ya kwamba sio wapigaji kura tu ambao wako katika eneo Bunge. Kwa mfano, wapigaji kura wanaweza kuwa elfu mbili lakini eneo Bunge lina zaidi ya watu laki tatu au tano. Inategemea namna ambayo watu watajitokeza kupiga kura. Wanaweza wasijitokeze kwa wingi na isichukuliwe kwamba wale watu elfu tatu waliojitokeza kupiga kura ndio wanawakilisha watu laki tano. Isikuwe ni lazima nafasi zipewe kwa hao watu tu na je, wale wengine watafanyaje? Wao pia ni Wakenya na wanastahili pia kupata hela za kuwasaidia. Spika wa muda, ni muhimu tupate Mawaziri ndani ya Bunge ili ukiuliza swali linapo kosa kujibiwa vizuri, basi kuna nafasi ya kuuliza maswali ya ziada. Vile vile, swali likiulizwa huwa halijalenga eneo Bunge moja bali maeneo Bunge kadhaa. Hivyo basi, wahusika wa maeneo Bunge mengine pia watapata nafasi ya kuuliza maswali ya ziada ikiwa Waziri atakuwa hapa ndani. Ninaona kuwa tutakuwa na mwelekeo mzuri hivyo basi ninaunga mkono urekebishaji wa Katiba ili mambo haya mengine yote yaweze kuzingatiwa. Mhe. Spika wa Muda, ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii."
}