GET /api/v0.1/hansard/entries/1220454/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1220454,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220454/?format=api",
"text_counter": 60,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nauunga mkono dua lililoletwe na Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge hili. Masuala ya shamba ni nyeti na yamekuwa yakiathiri watu hapa nchini. Wakipsigis walionyang’anywa mashamba yao wanaishi maisha ya kichochole ilhali yale mashamba ni yao. Ukitembea sehemu nyingi katika Kaunti za Nyeri, Kiambu, Murang’a na Laikipia unapata wakaazi ambao walikuwa na shamba zao kitambo, lakini wakoloni walipowasili waliwafukuza na kuwatimua katika vijiji. Watu wale walibaki kufanya kazi katika mashamba waliyonyang’anywa. Hivi leo, watu hao hawajapewa fidia na bado wanaendelea kusononeka na kupata majanga."
}