GET /api/v0.1/hansard/entries/1220468/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1220468,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220468/?format=api",
    "text_counter": 74,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika. Pia nitaongea kwa Kiswahili kama mwenzangu Sen. Kinyua wa Laikipia. Kwanza, ninampa kongole Kiongozi wa Wali Wengi kwa kuleta Mswada huu ambao unahusisha jamii ya Kipsigis. Pia sisi mahali nimetoka, Kirinyaga, tuko na tabu pia ya mashamba lakini yetu ni tofauti kidogo. Eneo la Mwea wakati wa ukoloni lilikuwa limefanywa jela ya wale watu waliokuwa wanapigania Uhuru. Baada ya uhuru kupatikana, watu wa Kirinyaga na wengine, waliwawachwa katika yale mashamba ambayo mpaka wanaishi kama wenyewe lakini sio wenyewe kwa sababu bado hawajapewa hati miliki. Serikali yetu ya Kenya Kwanza inazingatia na kuhifadhi heshima ya mahuluku taabu ambao wanaitwa kwa Kiingereza hustlers . Nyanya yangu alikuwa anaishi pale hadi kufa kwake akiwa na miaka 115. Hadi sasa, jamii zinazoishi pale zimezaana na kuzikana lakini babu za watoto ambao wamezaliwa pale hawakuwa na hati miliki. Kwa hivyo, vita nyingi ambazo zinatokea pale ni kwa sababu watu wanapigania mashamba amabayo hayawezi kugawika, na hati miliki hazijawahi patikana. Vile, kuna mashamba ya South Ngariama na Mwea Irrigation Scheme ambazo hati miliki hazijawahi kupatikana. Tukizingatia Serikali ya Kenya Kwanza, tukipawapa hati miliki wale ambao tayari wako katika mashamba yao, wataweza kujiendeleza. Pia tunapaswa kuangalia maslahi ya watu ambao hawakulipwa fidia kama Kipsigis na wale Mau Mau. Tunawafanyia haki na kurejesha heshima kwa watu ambao walihusika kutupigania Uhuru ambao mpaka siku ya leo tunaupigania"
}