GET /api/v0.1/hansard/entries/1220491/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1220491,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220491/?format=api",
"text_counter": 97,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13733,
"legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
"slug": "agnes-kavindu-muthama"
},
"content": "Karibu kila pahali Kenya kuna shida maana wakati tulipokuwa chini ya Wakoloni, walinyakua mashamba kila mahali. Pahali walipoona mashamba mazuri, waliyanyakua. Nikizungumzia juu ya Ukambani, kuna Street inaitwa Muindi Mbingu hapa Nairobi. Hao mpaka waleo wanakutana mahali wakidai ng’ombe wao ambao waliuliwa na hao masettlers . Wakati walisettle huko walileta ng’ombe aina ya freshians na wakasema wale ng’ombe wa locals, wote wauliwe kwa sababu wangeambukiza ng’ombe wao magonjwa na kuleta vifo. Kwa hivyo, ng’ombe wote waliokuwa katika maeneo hayo waliuawa. Baadhi ya hao watu walikufa na wengine wako hai. Wengine, wajukuu wao na vitukuu wanaendelea kudai ng’ombe wao. Kwa hivyo, inafaa hao watu wapate haki yao. Wale wanadai mashamba yao wapate mashamba yao na hati miliki. Wanodai ng’ombe pia wapate. Kuna wengine wa Mau Mau ambao walipoteza mashamba yao huko kwetu. Mpaka wa leo wanadai Serikali ya Kenya iweze kuwapatia sehemu waweze kuishi kama watu ambao walipokonywa kule ambapo walikuwa wanaishi. Ninaomba ile Kamati itakayokabidhiwa suala hili wafanye kazi kwa bidii ili tuweze kuona haki ikitendeka. Mara nyingi tunaleta Motions, Statements, Petitions na zinakaa sana bila kujibiwa. Mara nyingi hata miaka mitano inaisha. Mtu akirudi tena labda ndipo anakuja kuomba maombi hayo tena. Ninaomba Kamati tuwajibike tuweze kufanya kazi tunayostahili kufanya kwa haraka. Asante, Bw. Spika. Ninaunga mkono."
}