GET /api/v0.1/hansard/entries/1220502/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1220502,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220502/?format=api",
"text_counter": 108,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 380,
"legal_name": "Shakila Abdalla",
"slug": "shakila-abdalla"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa hii nafasi. Kwanza ninampongeza Kiongozi wa Wengi kwa kuleta huu Mswada nyeti. Swala la ardhi linagusia kila sehemu katika nchi hii yetu ya Kenya. Masikitiko ni kwamba swala hili linaendelea kushindikana kutatulika. Katiba mpya ilikuja na Tume ya Kitaifa ya Ardhi, ambayo inafaa kuzingatia na kusimamia shida za dhuluma za kihistoria za ardhi. Masikitiko ni kwamba, Tume hiyo imezembea. Wao ndio wamekuwa wakarabati wa ufisadi wa ardhi. Sasa hatuelewi hili tatizo litatatulika vipi. Watu wa Kaunti ya Lamu ndio walikuwa maskuota wa kwanza ambao walipigwa baada ya Kenya kupata Uhuru wakati wa mashifta. Hatujapata haki zetu mpaka kufikia leo. Vijiji 18 viliathirika na watu kusambaritika. Sasa hivi tunaitwa minority kwa sababu watu wetu walipigwa na wakasambaratika ulimwengu mzima. Ilikuwa kutokana na vita vya mashifta na ardhi yetu ikachukuliwa kupewa wasio husika. Ikiwa Serikali ina nia ya kutatua hili swala la ardhi, ni lazima iweke mikakati ya kuhakikisha wale waliodhulumiwa, wapatiwe hizo ardhi kwa njia mwafaka. Kuna watu ambao wanachukua fursa hiyo kudhulumu wanyonge ambao hawaelewi haki zao wala hawana njia na mbinu za kupata hati miliki. Wengine wanajifaidi kwa kujitolea hati miliki na kisha wanavamia ardhi za wengine na kudai ni zao. Kulingana na sheria, vitendo kama hivyo havifai kufanyika hapa Kenya. Unakuta mambo mengine yanatokea kwenye kaunti fulani, ambayo huwezi kuyaona kwenye kaunti zingine. Ni kwa nini kaunti zingine zinadhulumiwa haki zao, na zingine wanapewa kikamilifu? Kwa hivyo, tunaomba na tunataka shida hii itatuliwe kikamilifu. Hizi dhuluma ambazo zina---"
}