GET /api/v0.1/hansard/entries/1220508/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1220508,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220508/?format=api",
    "text_counter": 114,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Seki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13598,
        "legal_name": "Samuel Seki Kanar",
        "slug": "samuel-seki-kanar"
    },
    "content": "Walowezi wa Kiingereza walichukua mashamba katika kaunti nyingi kama vile Laikipia, Narok, Kajiado na hata sehemu kubwa ya Kaunti ya Machakos, ambayo Sen. Kavindu Muthama alizungumzia. Walichukua tu bila kuzingatia hali ya wenyenji wa kaunti hizi watafaidika namna gani. Ni vizuri kwamba Sen. Cheruiyot ameleta ombi hili ili tuweze kuingalia kwa kina. Kuna shida kubwa sana katika sehemu ya Kajiado ambayo mimi ninawakilisha. Sehemu inayoitwa Magadi iko na madini aina ya soda ash katika Wadi nzima. Hata hivyo, hawa Walowezi wa Uingereza wamemiliki hiyo Wadi yote kwa jumla na kukodisha. Hayo madini ya soda ash yanayotoka nchi hii kuenda katika nchi zingine. Jamii zilizoko katika sehemu hiyo hawafaidiki chochote. Hata Kaunti yenyewe, haipati faida. Serikali ya Kaunti haipati hata ile faida kidogo ya ardhi ambayo inatakiwa kupata. Mpaka sasa, Kaunti bado inataabika kutafuta zile rates kwa sababu hata wanakataa kulipa---"
}