GET /api/v0.1/hansard/entries/1220513/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1220513,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220513/?format=api",
    "text_counter": 119,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Kwa mfano, Shirika la Habari la BBC lilionyesha sinema fupi kuhusu gharama ya majani chai ambayo inauzwa katika nchi za kigeni. Makampuni ambayo yalinyakua mashamba haya, hujipiga kifua na kuendeleza udhalimu kwa kuleta mashine ambazo za kuchuna majani na kuwanyima wenyeji nafasi za kazi. Bw. Spika, ukoloni mamboleo hautakiwi kuwa unaendelea kamwe. Serikali ya nchi ya Kenya ndiyo ina haki ya kunyakua mashamba popote kwa mjibu wa sheria. Iwapo wenyeji walinyang’anywa mashamba kihistoria, mbona ni vigumu Rais William Ruto kuamka asubuhi na kuamuru mashirika kama Finlays, kuleta stakabadhi zao ili idhibitishwe iwapo walipata hayo mashamba kihalali? Mkataba wao ulikuwa upi? Kama mkataba huo haukuwa halisi, lazima mambo yabadilike. Mimi ninaamini, kama Bibilia ilivyosema, miaka iliyoliwa na nzige lazima irudi. Watu wa Kaunti ya Kericho ambao mashamba yao yalichukuliwa, lazima warejeshewe. Wale ambao wamekuwa wakivuna matunda ya wenyewe hapa Mlima Kenya na viunga vyake, vilevile Serikali ichukue hatua."
}