GET /api/v0.1/hansard/entries/1220543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1220543,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220543/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Bw. Spika, wanafunzi hawa ambao wamekaa hapa ndani ni miongoni mwa wanafunzi wenye tabia nzuri, heshima na ambao wamejipanga katika masomo yao. Shule hii ya Christ the King ni shule ambayo mtihani uliokwisha hivi majuzi ilitoa mwanafunzi wa kwanza Kenya hii. Ndio kwa sababu tukasema chanda chema huvikwa pete. Leo hii wamekaa hapa kujionea kama jinsi mwanariadha shupavu alisema binadamu hatimiliki na hana kikomo. Yote yawezekana chini ya jua na juu ya ardhi. Sisi viongozi wenu tunawapenda. Mkituona mjue yote yanawezekana. Tumetoka familia dogo chochole. Wazazi wetu hawakutambulika na yeyote lakini Mungu huyu halali. Machozi ya waja wake hayampiti hivi akitazama."
}