GET /api/v0.1/hansard/entries/1220545/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1220545,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220545/?format=api",
    "text_counter": 151,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Wanafunzi, mjionee hapa wale ambao mnawaenzi kwenye vyombo vya habari. Tuko na Mhe. Spika Amason Kingi, msomi na wakili. Tuko na Mheshimiwa Bonny Khalwale, jirani pale nyumbani. Tuko na aliyekuwa gavana, Mhe. Mandago na wengine wengi. Viongozi wanawake wako hapo wenye tajriba kubwa ambao kuja kwao hapa sio kwa kuvaa marinda ila yale yalio vichwani mwao. Sasa kuweni na imani kwamba Kenya hii ni yetu sote. Sisi kama viongozi tutahakikisha mnapata haki yenu. Tuliahidi masomo yatakuwa bure. Kama viongozi, tutasukuma Serikali ifanye jinsi tulikubaliana. Walimu mlioko hapa, tumejadili maswala yenu. Nyinyi ni wachapa kazi ambao mnachapa kazi mkilia, mkiuliza mungu mlikosea nini? Hivi leo, katika Seneti hii tumejadili na tutaendelea kujadili maswala ya walimu Kenya hii. Sasa msikate tamaa. Tunasababu ya kuishi na kuboresha Kenya. Muwe na Imani kwamba chini ya uongozi wa Mheshimiwa Jafason Kingi na viongozi wa Walio Wengi na Wachache na viongozi wa Kamati mbali, yote itawezekana. Bw. Spika, sitaki kupita hapo, ili niwape wenzangu nafasi kujivunia wanafunzi kutoka Bungoma. Mkirudi Bungoma waambie tuko imara. Mnaona jinsi tunafanya kazi. Msijihurumie au kusema laiti mngejuwa. Semeni tungejuwa mapema yangepita mapema."
}