GET /api/v0.1/hansard/entries/1220550/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1220550,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220550/?format=api",
    "text_counter": 156,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sifuna",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13599,
        "legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
        "slug": "sifuna-edwin-watenya"
    },
    "content": "Bw. Spika, mimi sio mtu wa kutishwa na lugha yeyote. Ninaweza kutoa Hoja zangu kwa lugha yeyote ambayo itamridhisha Kiongozi wa Walio Wengi. Ameniomba nitumie Kiswahili kwa sababu ndugu yangu, Seneta wa Bungoma, ana weledi wa lugha hiyo. Nitajaribu pia niweze kwenda katika nyayo zake. Bw. Spika, wengi wanajuwa mimi ni mzaliwa wa Kaunti ya Bungoma. Wakati ya likizo ya Krismasi baada ya sisi kumaliza ile shughuli ambayo ulikuwa umetupa, na ndugu zetu wa Meru, chini ya uongozi wa Sen. (Dr.) Bonny Khalwale wa Kakamega, nilienda nyumbani ili kuona wazazi. Wakati moja tumeenda katika kanisa la Christ the King ambalo ndio kanisa la babangu na mamangu. Katika sala za wakristo wa Kikatoliki, kuna wakati waumini wanapewa nafasi ya kusoma neno kabla muhubiri au father hajaubiri. Siku hiyo ilikuwa zamu ya watoto watatu. Moja anaitwa Sandra Nelima, mwingine Valencia Matiro na Kevin Otieno kusoma kabla Father hajasoma somo la kwanza na la pili. Niliridhika na kufurahishwa sana na jinsi watoto hawa walikuwa na uwezo wa kusoma Kiswahili kwa njia ambayo ilieleweka na waumini wote waliokuwa kanisani. Niliwachekesha kidogo nikiwaambia kwamba jinsi walivyosoma siku hiyo kuna Maseneta wengi sana ndani ya Bunge hili ambao hawawezi kufikia kiwango hicho. Niliwaaahidi kwamba nitawaalika wajionee wenyewe ili nisiwe kwamba nawaharibia wenzangu sifa. Kwa huo wito, ningependa umpe fursa Seneta wa Kisumu Mheshimiwa Profesa na umwambie azungumze kwa lugha ya Kiswahili pekee ili tuone kama anaweza kufika kiwango cha hao vijana. Mpe fursa rafiki yangu Seneta wa Homa Bay ambaye husema ‘Kiswahili sio mdomo chao’ ili hawa madada zangu wadogo waamini sikuharibia wenzangu sifa."
}