GET /api/v0.1/hansard/entries/1220552/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1220552,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220552/?format=api",
    "text_counter": 158,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sifuna",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13599,
        "legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
        "slug": "sifuna-edwin-watenya"
    },
    "content": "Ikizidi mpe Sen. Abass nafasi, yuko pale. Mtaona akiweka ‘ bahali yake.’ Bw. Spika, ninashukuru sana kwa kunipa fursa hii kuwakaribisha ndugu zangu na dada zangu katika Bunge letu hili la Seneti. Ninaamini wamepata fursa ya kuona jinsi ambavyo tunaendesha mambo yetu hapa. Ninawapa moyo kwamba jinsi nilivyoondokea sehemu hizo kuwa Seneta wa Jiji Kuu la Nairobi, inawezekana kwamba wao wakitia hekima na fora katika masomo yao, watajipata hapa siku moja wakihutubia taifa tunavyofanya hapa. Ninawatakia kila la heri. Safari njema mnaporudi nyumbani. Wasalamie wazazi wenu. Mimi ni mmoja wenu katika kanisa la Christ the King. Mnajuwa pia jumuia yangu. Wasalimu wote na waambie ninawapenda. Asante sana, Mungu awabariki."
}