GET /api/v0.1/hansard/entries/1220612/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1220612,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220612/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika. Leo tunakienzi Kiswahili. Ninasimama kuunga mkono Taarifa ya Sen. Munyi Mundigi. Hakika, Wakenya wanaumia sana kwa sababu ya stima. Wananchi wanalipa ili wapate umeme kwa matumizi yao ya nyumbani, viwandani na hata katika biashara zao. Basi stima inapokatwa au kupotea, wananchi wanaumia sana. Siku hizi, Kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini haieleweki kabisa. Wanasababisha mateso kwa wananchi badala ya kuwa msaada kwao. Kwa hivyo, Taarifa hii itakapofikia Kamati ya Huduma ya Nishati, inafaa waishugulikie kwa makini sana. Wakifanya hivyo, watasaidia Kaunti ya Embu na zinginezo nchini."
}