GET /api/v0.1/hansard/entries/1220614/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1220614,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220614/?format=api",
"text_counter": 220,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Joe Nyutu",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw. Spika. Na mimi pia wacha nizungumze Kiswahili kwa maana Sen. Wafula alikitanguliza kama lugha ya kuendeleza majadiliano yetu hivi leo. Bw. Spika ninasimama kuunga mkono Taarifa ya Sen. Munyi Mundigi, kuhusu ukosefu wa usambazaji umeme kwa muda mrefu. Kamati husika itakaposhughulikia Taarifa hii, ikiwezekana, waangalie jinsi tunaweza kupata kampuni zingine za kusambaza umeme. Ikiwa ni kampuni moja tu ndio itaendelea kusambaza nguvu za umeme, basi huenda shida hizi zitaendelea kuwa nasi kwa muda mrefu. Kwa hivyo, ikiwezekana, sheria inayoipa kampuni hii haki ya kipekee ya kuuza stima, ifunguliwe. Bw. Spika, katika historia ya biashara, huduma huwa bora zaidi kunapokuwa na washindani. Kwa hivyo, ninapendekeza pawe na wengine ambao watashindana na kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini."
}