GET /api/v0.1/hansard/entries/1220619/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1220619,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220619/?format=api",
"text_counter": 225,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika, nasimama kuunga mkono Taarifa hii iliyoletwa na Seneta wa kutoka Embu. Shida kubwa ilioko kulingana na vile nimesikia ni kwa sababu ya ukiritimba. Unapata ya kwamba Shirika la Nguvu za umeme, Kenya Power, ndio wenye jukumu ya kusambaza nguvu za umeme katika nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo, wanafanya mambo kiholela vile ambavyo hawapaswi kufanya bila kuwa na mtu mwingine aliyekatika hali ya mashindano nao. Kwa hivyo, naomba Kamati ya Kawi ambayo inaongozwa na Sen. Wamatinga, waweze kujizatiti na kuwauliza maswali magumu. Tunafaa kuwa na kampuni zingine ambazo zinaweza kuchukua fursa ile na kusambaza nguvu za umeme ili kuwe na hali ya ushindani na hawa ndugu zetu wa Kenya Power . Kampuni ya Kenya Power wako pekee yao, ndiposa kunakuwa na hiyo shida ya ukiritimba na unapata wanagandamiza Wakenya. Kama vile viongozi wengine walivyoongea wamesema, vitu vinaharibika wakati vimewekwa kwenye majokofu. Watu wanapata shida wakiwa hospitalini na hakuna fidia yoyote Shirika la Nguvu za Umeme inawapatia Wakenya. Kwa hivyo, ningeomba Mwenyekiti kwa sababu yuko hapa na ninamjua yeye ni mchapa kazi, sina shaka rohoni atalishughulikia jambo hilo kwa hali ya dharura na atatupatia jawabu la kuduma badala ya sisi kila wakati kuongea haya mambo ya hawa ndugu zetu wa Kenya Power . Ni kanakwamba wamekuwa ni kama sikio la kufa ambalo halisikii dawa wala mtekamaji msikitini. Asante, Bw. Spika."
}