GET /api/v0.1/hansard/entries/1220653/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1220653,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220653/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Bw. Spika, umeme ni jambo ambalo ni muhimu sana katika ukuzi wa uchumi wa Jamhuri ya Kenya. Tunapoendelea kupatwa na majanga ya ukosefu wa umeme katika sehemu mbalimbali za Jamhuri ya Kenya, unaona kwamba kunazoroteka zaidi katika upande wa maendeleo ikizingatiwa pia kwamba hospitali zetu zinahitaji umeme kila siku. Mimi nikiongelea kuhusu Kaunti yangu ya Lamu, niko na kisiwa ambacho kinaitwa Faza. Faza ni kisiwa ambacho sana sana wakaazi wa pale wanategemea uvuvi. Wakati ambapo stima inakosekana kama vile sasa, muda wa mwezi mmoja, Faza imekosa stima. Wale wavuvi ambao kitega uchumi chao ni kuvua, lazima waweze kuwa na barafu ambayo inawasaidia katika kuhifadhi zile samaki zao. Wakati ambapo umeme unakosekana katika ile sehemu ya Lamu ama kisiwa cha Lamu, inakuwa shida kubwa sana. Tumekuwa na janga hilo katika muda wa mwezi mmoja. Nataka nichukue head"
}