GET /api/v0.1/hansard/entries/1220655/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1220655,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1220655/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Githuku",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13595,
        "legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
        "slug": "kamau-joseph-githuku"
    },
    "content": "kama vile Sen. Wamatinga ameweza kusema kwamba hili Shirika la Kenya Power linafaa lichukuliwe head on kuona kwamba wakati wowote limeweza kujukumika katika mambo ya kulipia watu fidia wakati ambapo wanasababisha hasara kubwa kwenye uchumi wa watu wetu. Bw. Spika, Kisiwa cha Faza ni sehemu ambayo mpaka sasa, haijakuwa connected na national grid. Wanatumia jenereta kuweza kuleta stima katika ile sehemu. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba watu wangu wa Lamu wamebaki nyuma kwa muda mrefu. Ndiposa saa hii, ningetaka kusema kwamba serikali inafaa ijukumike Zaidi ione pia kwamba imeweza kuconnect Lamu na national grid ili wakati wowote, stima iwe ikipatikana mahali pale. Hii ni kwa sababu watu wangu wanapotumia jenereta, inakuwa pia ni shida kuvukisha ile mafuta ama dizeli ambayo inatumika kuendesha ile jenereta katika ile sehemu. Bw. Spika, naunga mkono."
}