GET /api/v0.1/hansard/entries/1221090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1221090,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1221090/?format=api",
    "text_counter": 188,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, nina kushukuru kwa kunipa fursa hii. Vile vile, ninamshukuru Sen. Cherarkey kwa kuleta swala hili nyeti ya udhamini wa wanafunzi. Udhamini wa wanafunzi umekuwa ni jambo nzuri sana. Lakini, wale ambao ni wakora wanachukua fursa ile kujinufaisha wenyewe kwa sababu wanajua wanafunzi wengi hawana uwezo. Ukiwatajia udhamini, ni watu ambao wanataka masomo. Lakini, kwa sababu ya ukosefu wa pesa, kunafanywa mchango. Unapata hata wale ambao wanaishi katika maisha ya uchochele wanafanya harambee kusudi waweze kupata ule udhamini na kupeleka watoto wao shuleni waweze kupata masomo. Bw. Spika, Kamati ambayo itashughulikia jambo hili, inapaswa ilete mwangaza zaidi watu wajue Serikali ama Wizara ya Elimu ni hatua zipi ambayo inachukua kusudi Wakenya wawache kulaghaiwa wakiwa wanatafuta udhamini. Hii ni kwa sababu Wakenya wanataka masomo na wanajua kwamba watapata masomo ya kiwango cha juu pengine wakienda katika nchi za ughaibuini. Kwa sababu ya umaskini, mtu yeyote akisema atawadhamini wanafunzi, watu watauza mbuzi na kuku kwa minajili ya kupata ule udhamini. Kwa hivyo, Kamati ambayo itapatiwa hili jukumu isiangalie tu sehemu hiyo ya Uasin Gishu. Isiangalie tu Taarifa iliyoletwa. Iangazie hayo mambo kwa kindani ndiyo waweze kuleta suluhu la kudumu. Tusiwe kila wakati tunaongea kuhusu hili jambo. Kwa sababu ya ufukara wananchi walionao, wanaweze kuhadaiwa na walaghai ambao wanachukua kila fursa ilioko. Si fursa ya kuwaajiri watu au ya kuwadhamini wanafunzi. Walaghai wanachukua fursa yeyote ambapo watu wanachechemkia jambo, kuwalaghai wananchi wa Kenya. Bw. Spika, ninaunga mkono na kuomba Kamati ambayo itashughulikia jambo hili, ishughulikie kwa kindani na waweze kutupatia suluhu la kudumu. Ninashukuru."
}