GET /api/v0.1/hansard/entries/1221129/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1221129,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1221129/?format=api",
    "text_counter": 227,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa nafasi hii. Ijumaa na Jumamosi tulikuwa na kikosi cha Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kule Kaunti ya Kitui. baadhi ya maswali ambayo mwenzangu Spika ameuliza ni maswali ambayo wakulima wa ndengu waliuliza. Kwa mfano, ni mbolea mifuko mingapi ambayo imeletwa maeneo hayo na ni vigezo vipi waliotumia kuwapa wakulima mbolea hiyo? Katika kumbukumbu na vitabu vya wataalam wa kilimo, ekari moja ya shamba iwapo ni la mahindi huhitaji magunia kadhaa ya mbolea. Wanayosema yameafikiwa na Idara ama Kilimo ama hii ni mbolea ambayo imekuwa inapeanwa tu kwa minajili ya kukimu kiu cha wakulima Kenya? Hoja ya pili - kuna maeneo ya magala nchini ambayo Serikali imeagiza mbolea kupelekwa. Wakulima wanapochukua mbolea hii wanaitishwa pesa au la? Nimekuwa nikizungumza na mkulima mmoja kutoka eneo bunge la Bumula ambaye alienda kuchukua mbolea kwa pesa zilizostahili lakini akaelezwa ili alihifadhi gunia lake la mbolea lazima angetoa shilingi 85. Iwapo wakulima maskini watakuwa wanaitishwa pesa kidogo kama hizo tutaweza kuyaafiki malengo ya Serikali? Kuna maeneo humu nchini ambamo panajulikana kwamba ni vikapu vya chakula. Ni magunia mangapi ya mbolea yamefika kule? Mfano kaunti za Trans-Nzoia, Bungoma, Uasin Gishu, Kakamega na Kisii. Maeneo ambayo mahindi na vyakula vingine vya kushika tumbo vinatoka. Si vya mzaha vinavyopoteza muda."
}