GET /api/v0.1/hansard/entries/1221251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1221251,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1221251/?format=api",
    "text_counter": 349,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Katika maeneo mbalimbali humu Kenya kuna ukataji miti katika maeneo ambayo yametajika jinsi ulivyosikia. Nadhani ni mpango ambayo mabepari wa kisiasa wako nao kuhakikisha maeneo fulani humu nchini yanapoteza uridhi wake. Kwa mfano, misitu ya Kaimosi, kiitikadi na kijamii, mila na desturi za Watiriki hufanyika katika misitu hii. Haiwezekani kupata watu kuja tu na mashine kukata miti pasipokubaliana na washikadau maeneo haya. Pia, misitu ya Malava na mlima Elgon. Ninaomba kwamba, iwapo kuna njama ya Serikali ama wale waliomo serikalini na mafidhuli wanabiashara, sisi kama Maseneta kutoka maeneo yetu tupambane na wao kule mashinani. Kama Seneta mwenzangu alivyouliza, itakuwaje miti ikatwe na hakuna upanzi wa miti unaoendelea hadi sasa? Ni Kenya gani tunaishi ambamo mtu amekaa katika mji wa Nairobi anatia sahihi barua ya kukata miti Kaunti ya Nyanza. Mwenyewe hajui watu wa Kaunti ya Nyanza wanaishi namna gani, wameumia vipi, wana uhusiano upi na miti ile na mazingira haya? Ninaomba Serikali na Seneti hii kwamba iwapo sisi kama Serikali tumeamua kwamba tunapanda miti, haipaswi mpaka sasa, tusikie watu wanaenda misitu yetu kukata miti ilhali hata ule mwito ambao Rais ametoa, hatujafika nusu ya yale ambayo tunaahidi Wakenya kwamba tutapanda. Ninaomba Seneti na Kamati inayohusika na misitu na mali asili, tujikite katikati ya mambo haya na tuhakikishe kwamba urithi wa watu wetu ambao umelindwa kwa miaka na mikaka, haushambuliwi na watu ambao wanaona pesa pekee. Hawaoni maisha ya wanyama pale ndani, urithi wa kitamaduni pale ndani na uboreshaji wa mazingira na hewa safi katika maeneo yetu. Nikimalizia, hii ndio miti imetusaidia sisi watu wa mkoa wa magharibi na bonde la ufa kupata mvua wakati unaostahili. Iwapo tutaikata, awamu yetu ya siasa sasa, siku zijazo, tutaambia watu wetu kwamba tuliungana na mafedhuli kukata miti kwa sababu ya matumbo yetu. Mimi ninapinga na ninahusiana kabisa na Hoja ya Sen. Osotsi. Hatutakubali miti ambayo ilipandwa na mababu zetu kushambuliwa na watu ambao hawakuwepo lakini njaa imewaleta kwetu. Tutapambana nao kwa udi na uvumba."
}