GET /api/v0.1/hansard/entries/1221359/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1221359,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1221359/?format=api",
"text_counter": 53,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "(PPDT) - walitangaza matokeo ya wale waliopeleka zile kesi mbele yake. Matokeo hayo yako wazi. Wananchi wote nchini Kenya wanajua ya kwamba walijitoa na wakasema kwamba wao hawana haki ya kuangalia hiyo kesi. Bw. Spika, sasa, jukumu ni lako kuliweka wazi, kwa sababu taarifa hiyo si geni kwako, kwa hawa Seneta wenzangu na taifa nzima la Kenya. Politcal Parties DisputeTribunal (PPDT) walikaa na wakajitoa. Walisema kwamba wao hawana uwezo wa kuinglia ratiba yoyote inayoendelea ndani ya Bunge la Seneti. Bw. Spika, kwa hivyo, tunategemea Mawasiliano kutoka kwa kiti kikubwa ulichoketi. Katika harakati zako na hekima, najua unaweza kuona kwamba ni ukweli uongozi wa upande wa Walio Wachache hauko kamili na umeendelea kuzoroteshwa kwa sababu ya uamuzi ambao tulikuwa tunaungoja. Tumeungoja kwa wiki tatu sasa, na niko na matumaini kwamba mwangaza umeonekana. Hata ndugu yangu, Sen. Cheruiyot, anakubaliana na mimi kwamba alisikia matangazo hayo na anajua hayo. Sote tulio hapa kama Maseneta, tunangoja na anafurahia. Utaona, Bunge hili litajaa sasa. Asante sana Bw. Spika."
}