GET /api/v0.1/hansard/entries/1221517/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1221517,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1221517/?format=api",
    "text_counter": 211,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, ninasumbuka kwa sababu tayari wewe ulikuwa umefanya uamuzi kwa jambo hili. Karatasi iliyoletwa hapa na ndugu yangu mwana sharia, Sen. Omogeni, hayo ndio mambo anakuambia ufanye uamuzi. Wewe mwenyewe unajua ni wakati gani utafanya uamuzi, ni mambo gani utaangalia uweze kufanya uamuzi. Hakuna mtu yeyote katika Bunge hili anaweza kukushurutisha, kukuamrisha ama kukuambia chochote kwa sababu wewe ndio mwenye uwezo na ujuzi wa kufanya hiyo kazi. Na kwa sababu ulikuwa umefanya uamuzi, na umeletewa barua ambayo wewe haujui imetoka wapi. Imesemekana imeletwa siku ya leo. Bw. Spika, wewe unapaswa kufanya uamuzi bila kuamrishwa na mtu yoyote. Lakini mimi nimekaa hapa, ninaona kama vile unavyoongoza Bunge hili, kidogo niko na tashwishi. Hii ni kwa sababu watu wanapoongea, nimemwona Seneta wa Nairobi, Sen. Sifuna, akifanya vile ambavyo inakubalika kisheria. Nimeona leo pia Seneta wa Narok na Sen. Wambua wamekuwa watulivu. Ukitembea katika Bunge zingine za duniani kama ni Afrika Kusini, Australia na Uingereza, haya si mambo ya kuongea bungeni. Bw. Spika, watu wakubaliwe waongee katika Bunge. Lakini, nina uoga kidogo wakati mtu akiongea kidogo, unamwambia utamfukuza."
}