GET /api/v0.1/hansard/entries/1221519/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1221519,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1221519/?format=api",
"text_counter": 213,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika tumetembelea nchi zingine ambazo tunaziiga, na tukaona vile wanavyojadili. Wakati mwingine tunapojadili, jadhba inapokupanda unapaswa kusema jambo ulilonalo. Lakini, ikiwa unatuogofya na kutushtua, basi mijadala yetu itakuwa inachechemea. Bw. Spika, ninakuomba usimame na uamuzi uliotoa kwa sababu tumekaa wiki tatu bila ndugu zangu wa upinzani. Hata wiki ya nne na tano ni sawa. Wangoje ufanye uamuzi wakati utakapotaka, kulingana na Kanuni za Bunge hii. Bw. Spika, ninashukuru."
}