GET /api/v0.1/hansard/entries/1221530/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1221530,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1221530/?format=api",
    "text_counter": 224,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Itakumbukwa kwamba wiki tatu zilizopita, Sen. Orwoba, alikuwa hapa Bungeni akiwa ameingia katika hada zake. Sisi kama Maseneta tulimheshimu na tukamvumilia katika ile hali aliyokuwa nayo. Leo ni masikitiko kwamba, Sen. Orwoba anaweza kusimama katika Bunge hili na kukemea haki ya Maseneta wa upinzani, wakidai haki zao. Bw. Spika, mambo mengi yamezungumzwa. Nimeskia pia Kiongozi wa Walio Wengi akisema kwamba, tunaharibu wakati wa Bunge. Lakini, haki ni haki. Haiwezekani kwamba haki zetu sisi zikataliwe katika Bunge tuliochaguliwa kuwakilisha watu wetu. Ikiwa sisi kama Seneta, haki zetu zinakataliwa, je, itakuwa vipi kwa wale ambao tunaowaakilisha? Bw. Spika, ruling imeletwa mbele yako. Sasa, ninataka kukukabidhi order iliyotolewa kuambatana na ruling ya korti. Tafadhali niruhusu."
}