GET /api/v0.1/hansard/entries/1221665/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1221665,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1221665/?format=api",
"text_counter": 359,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ukisoma kitabu--- Ni vizuri ijulikane ya kwamba viongozi ama mashujaa huchipuka wakati kuna janga na wakati huu kuna janga. Mimi ni mmoja wa Kamati hii ya Barabara, Uchukuzi na Makazi. Tulipata ujumbe kutoka kwa Seneta wa Homa Bay akisema ya kwamba ombi lililokuwa limeombwa na sisi tulikuwa tumejitayarisha kuendelea na haya maneno kwa sababu ya muda uliowekwa. Japo, Sen. M. Kajwang akatuambia kunaweza kuwa na mvutano na vurugu. Ni vizuri kwa sababu hakutaka tujipate katika hali ya sinto fahamu wakati tukifika huko. Lakini tumekuwa tukisema kila wakati tutatembea pale, kunakuwa na sababu ambayo inatuzuia kufanya kazi yetu. Hata ijapokuwa anasema kutakuwa na maandamano, na ninataka kukubaliana na Kiranja wa Walio Wengi ya kwamba Seneta rafiki yangu Sen. M. Kajwang sio afisa wa usalama. Yeye hafanyi katika idara ile. Kwa hivyo, ijulikane wazi hakuna Seneta yeyote hawezi kuzuiwa kufanya kazi yake ya uangalizi na mtu yoyote. Nakumbuka Bunge lililopita aliyekuwa Waziri wa Usalama Mheshimiwa Matiang’i alisema hatutakwenda Laikipia kwa sababu ya ukosefu wa usalama. Lakini tukasema, liwalo na liwe. Nataka kumpongeza Sen. Wetangula. Alisema ya kwamba Seneta hawezi kuzuiwa kufanya kazi yake hata kwenda kuangalia zile sehemu ambazo zina shida ni kazi yake. Sen. M. Kajwang’, nilitaka twende Mbita, Mfangano, tuone kama maandamano yamefanywa kama vile ulivyotaka. Hiyo ni kazi yetu. Tunataka kwenda kufanya kazi yetu. Hatuwezi kuzuiliwa. Bw. Spika wa Muda, ningependa kupongeza Mwenyekiti kwa sababu kama hatungefanya kazi yetu na muda unaendelea kuyoyoma, tungekemewa na kukejeliwa kama Kamati, ya kwamba hatufanyi kazi yetu. Mwenyekiti alikuja kusema kwamba muda uliotupa wa siku sitini unayoyoma. Hatuwezi kaa kitako halafu tukuje kusomewa ndani ya Seneti. Seneta alisema kwa mtandao wa Kamati yetu kwamba kutakuwa na vurugu na mvurutano. Kwa hivyo, Mwenyekiti alifanya inavyopaswa. Tumekuwa tukisema hayo. Ninakumbuka Sen. M. Kajwang’ alinipongeza nilipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ugatuzi, kwa sababu kila wakati nilikuwa nikileta Ripoti ya vile Kamati inavyoendelea."
}