GET /api/v0.1/hansard/entries/1221700/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1221700,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1221700/?format=api",
"text_counter": 394,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, ingekuwa bora kama ungenitetea kwa sababu hawa Maseneta wanaongea ninapozungumza ili usisikize kile ninachosema. Kanuni hizi zetu ni Kanuni za Kudumu na hizo ndio tunafuata. Lakini leo cha ajabu ni kwamba nilipopinga kwamba hatuwezi kuongea habari za Sen. M. Kajwang’, mwenyekiti aliyokuwa ameketi hapo saa hizo - na mashahidi wangu ni Sen. (Dr.) Lelegwe na Sen. Kinyua - alikiuka sheria. Ni jambo la aibu kuona Seneta mwingine anaweza kusimama hapa mbele ya watu kutoka sehemu mbali mbali za Taifa--- Ikiwa mimi ninaweza kusimama hapa na ndugu yangu wakili yuko hapa, alafu niongee juu yake kwa njia ambayo sio sawa ili Wakenya wengine wapate kujua. Mimi ninawaheshimu sana Sen. Wakili Sigei, Sen. (Dr.) Lelegwe na Kiranja wa walio Wengi. Sijawahi kuskia hata siku moja kwamba Kiranja wa walio Wengi amefanya tabia kama hiyo. Ingekuwa vizuri kama sisi hatungeingiliana hapa. Tufundishane heshima. Ahsante."
}