GET /api/v0.1/hansard/entries/1221790/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1221790,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1221790/?format=api",
    "text_counter": 484,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "ninavyofikiria kwamba wale walio nyumbani na wale wanafunzi ambao wanakuja hapa wanaona mtu kama Sen. (Dr.) Khalwale, wanamwona Sen. Madzayo, Sen. Cheruiyot, wanaona kijana shupavu, Sen. Wakili Sigei, tukiwa tunarushiana maneno kama hayo. Bw. Spika, kwa yote, piga moyo konde yaweke nyuma. Ninajua katika ile hasira ukiwa kinara katika hii Seneti unaweza kutoa uamuzi kuhusian na ile hasira iloyokuja kwa ghafla na wewe ni binadamu. Hakuna mtu anayeweza kukuita hivyo na wewe usimwite. Yeye akiwa ameenda kidogo upande ambao umezidi, mimi ningeomba hiyo. Hata pengine vile ulivyotamka pengine ulisema ilikuwa katika spur of the moment. Hata hivyo, yote hayo tuliyoyafanya, nimi ninasema tuyaweke nyuma tugange yale yanayokuja. Kwa ndugu zangu, mimi ninaweza kusema, kwa pande zote mbili, lazima tuonyeshe mfano. Kila siku, watu wanakuja hapa wakituona. Wanaoketi pale, wanaoangalia ndani ya nyumba kwa runinga, wanaoangalia katika ma-hall makubwa makubwa, sisi kama mfano, please, I plead with you, let us use good language. Let usParliamentary Language so that we can at least save this House. Pole, ninatumia lugha mbili. Lakini tunaendelea kudidimia kiheshima. Ningesema zote tuwe kitu kimoja ili tuweke heshima ya Sene ti k wa sababu sio sisi peke yetu wa mwisho kukaa hapa ndani. Vizazi na vizazi vitakuja kukaa hapa Ni lazima tuweke msingi wa heshima nzuri tunayopeana katika Seneti."
}