GET /api/v0.1/hansard/entries/1222042/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1222042,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222042/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Mimi pia nitoe risala zangu za rambirambi kwa familia ya aliyekuwa dada yetu, Mhe. Grace Onyango ambaye kule Nyanza alijulikana kama Nya’ Bungu yaani ‘Daughter of the Bush’. Mwanamke huyu amekuwa kielelezo chema sana katika uongozi wa akina mama haswa uongozi wa kisiasa. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa Meya katika Kaunti ya Kisumu baada ya kumrithi Mathias Ondiek. Alikuwa Spika kwa muda mfupi. Aidha alikuwa Naibu Spika kwa muda mrefu. Tunajua alikuwa katibu mkuu wa Muungano wa Waluo. Kwa hivyo, mama huyu alikuwa mfano bora kwa akina mama. Alionyesha kwamba tunaweza kuingia katika uongozi. Wakati wake kama kiongozi, akina mama walikuwa hawaonekani kabisa katika nyanja za uongozi tena katika kiwango cha kufanya maamuzi ya kisiasa. Mama huyu alijitosa katika ulingo wa siasa kupambana na akina baba. Wakati huu tunayo affirmative action ambayo imewekwa kusaidia akina mama. Wakati huo ulikuwa mgumu kwani tamaduni na dini zetu zilikuwa zinapinga kabisa uongozi wa akina mama. Lakini yeye alikuwa kielelezo na akaweza kuingia katika uongozi. Hakika, wasifu wake una sifa nzuri nzuri. Kama akina mama, tutauendeleza wasifu wake na tunajua vizazi vyetu vinavyokuja pia vitaelewa kuwa uongozi ni wa jinsia zote mbili; kike na kiume. Tunajua kuna mambo mengi yanayomkumba mama."
}