GET /api/v0.1/hansard/entries/1222075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1222075,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222075/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Asante Bwana Spika, kwa kunipa nafasi ya kutoa rambirambi zangu kwa niaba yangu, watu wangu wa Lamu East, na familia yangu, kwa familia ya Grace Onyango. Kwa kweli, Bi. Grace alikuwa mfano mwema. Mwanzo, ningependa kumpongeza Mbunge wa kiume ambaye ni rafiki wa wanawake. Inaonyesha kuwa kuna wanaume ambao ni marafiki wa wanawake. Lakini kuna wale ambao ni maadui wa wanawake ilhali hawawezi kukaa bila wanawake. Wakija hapa, wanaanza kutupiga. Hawawezi kukaa bila wanawake lakini wanapinga affirmative action . Tunavyo hivi viti 47 mkononi. Wanaume, msijisumbue kuvitoa. Hatuwezi kuwachilia kile tunacho ili tutafute kingine. Tumeona umuhimu wa affirmative action seats . Wengi wetu tulianza na affirmative action seats ndiyo tukaweza kupigania ubunge. Kwa hivyo, hakuna haja ya kujisumbua. Wale wanaume ambao wamesaidiwa na handbags hapa Bungeni wajifunze. Wakati mwingine wanatokwa na makamasi na hawana kitu cha kujifuta nacho kisha wanatolewa handkerchiefs au serviettes vinawasaidia. Wajifunze."
}