GET /api/v0.1/hansard/entries/1222730/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1222730,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222730/?format=api",
"text_counter": 364,
"type": "speech",
"speaker_name": "Molo, UDA",
"speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Spika wa Muda, kwa kunipa muda huu kuchangia Ripoti hii ambayo imeandaliwa vilivyo na rafiki yangu Mbunge wa Nakuru, Mhe. Gikaria. Hii Hoja Maalum ni ya kupitisha wanachama wa Baraza la Nchi la Mabadiliko ya Tabianchi, ama ukitaka, climate change . Mambo ya tabianchi yanahusisha unyevuanga, ama ukitaka kwa kimombo, humidity ; mambo ya kanieneo angahewa, ama ukipenda, atmosphericpressure ; mambo ya upepo; mambo usimbishaji, ama ukitaka precipitation; na masuala mengine yanayoathiri mambo ya hewa. Mambo mengi yamebadilika katika nchi yetu ya Kenya. Mahali ambapo natoka katika Eneo Bunge la Molo, hatujawahi kukaa miezi minne bila kupata hata tone moja la mvua. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba leo asubuhi na jana usiku kumenyesha mvua kwa mara ya kwanza baada ya miezi minne. Haya masuala ya tabianchi yalizungumziwa kule Marekani na aliyekuwa Rais Barack Obama na watu wengi walisema kwamba ni stori tu na mambo ambayo hayatakuja. Lakini tunapoangazia yale mambo ambayo yamebadilika wakati huu, kama vile mifugo wetu kufa kwa sababu ya kukosa nyasi na chakula, ni thibitisho kwamba haya masuala sasa yako pamoja nasi. Nashukuru Kamati hii kwa sababu ya kumkataa huyu mama, Umra Omar. Wakati nilijaribu kuzungumza na wanachama wa hii Kamati na kuwauliza ni kwa nini wanapendekeza tuwapitishe Emily Mwende Waita, John Kioli Kalua, na Prof. George Odera lakini tusimpitishe Umra Omar, walinieleza kwamba kabisa hakuonekana kama alielewa mambo ya tabianchi hata kidogo. Alipoulizwa kuhusu mambo ya hali ya fedha – kwa sababu ili uweze kuongoza Baraza kama hili, lazima uwe na uzoefu na ujuzi wa masuala ya uongozi na fedha – Mama Umar Omar hakuwa tayari kujibu. Hata zile karatasi ambazo alistahili kuleta kutoka kwa mashirika mbali mbali ya serikali ya uchunguzi, hakuwa nazo. Hivyo, itakuwa funzo kwa wote wanaoletwa katika Bunge hili kwamba haitoshi jina lako kupeanwa lipitishwe na Kamati yoyote kwa jukumu lolote katika nchi yetu ya Kenya. Kwamba Bunge la Kumi na Tatu ni Bunge ambalo litaangazia wote na kuangalia wale ambao wamehitimu kupitishwa katika hili Bunge. Kwa wale ambao hawatahitimu, hatutasita kamwe kuhakikisha tumewarudisha kwa raia ili tutafute Wakenya walio na ujuzi unaohitajika kufanya kazi ambazo wanapewa. Kwa hayo machache, naunga mkono Ripoti ya Kamati hii ambayo inaongozwa na Mhe. Gikaria. Asante Spika wa Muda."
}