GET /api/v0.1/hansard/entries/1222841/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1222841,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222841/?format=api",
    "text_counter": 475,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii. Mabadiliko ya anga ni mabadiliko ambayo yametutatiza kwa muda mrefu, haswa kwa maswala ya kilimo kwa ukosefu wa mvua. Tumetatizika sana. Pamoja na hayo, japo naunga mkono Hoja hii ya kwamba tuwapitishe hawa na tumkatae Umra Omar. Ttatizo langu kuu ni tukiwa tunahitaji watu walio na tajriba; je hii tarjiba wataitoa wapi pasipo kuwa kwa kazi ili waweze kupata hii tajriba na ujuzi? Kamati imemkataa lakini ningeomba tuzingatie kuwa wakati mwingi, sio rahisi kupata tajriba ukiwa kwenye masomo. Ni sharti utoke shuleni na uajiriwe ili uweze kupata tajriba ya hiyo kazi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}