GET /api/v0.1/hansard/entries/1222869/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1222869,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222869/?format=api",
"text_counter": 503,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Mhe. Spika wa Muda, Umrah ana tajriba ya mambo ya mazingira. Hayo ndiyo mambo yake. Ana shirika linaloitwa Safari Doctor, shirika ambalo limekuwa Lamu na limetusaidia sana mpaka likapewa tuzo na United Nations (UN) katika mambo haya. Leo, nashangaa ninapoambiwa kwamba Umrah hana tajriba. Umrah ndiye mtu anayeweza kututetea tupate fedha kutoka kwa donors ili zitusaidie kwa mambo ya mazingira. Rekodi zinaonyesha Umrah alishindana na nchi nyingine kwa mambo haya, akashinda kama Mkenya, na akapewa tuzo ya UN. Inasikitisha sana. Au ni kwa sababu yeye ni Mbajuni? Hizi shida ambazo tunapata ni nyingi. Mambo haya yamefanywa kana kwamba hawakuwa wanataka kumpatia hii nafasi. Pengine ana matatizo yake. Ni mtu amejieleza. Kama Wabunge wanasema alikuwa hataki, alikuja vipi mbele ya Kamati? Kamati ilimwambia alete stakabadhi izimiliki kwa kuwa hawakutaka alizopeleka IEBC. Alirudi na akahakikisha zimeletwa Bungeni. Kama alikuwa hataki, angefanya hayo vipi? Kabla ya saa sita, Umrah alikuwa ameleta hizo documents zote. Haya ndiyo mambo yanayofanyika. Wacha Wakenya wajue kwamba sisi Wabajuni wa Lamu tunakandamizwa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}