GET /api/v0.1/hansard/entries/1222884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1222884,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222884/?format=api",
"text_counter": 518,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Spika wa Muda. Hili ni Baraza muhimu sana ambalo linatakikana tulitengeneze kama Wakenya, hasa tukiangalia mabadiliko ya hali ya anga na mambo ya kiangazi tuliyo nayo. Hivyo basi, ni mwafaka kama Ripoti hii ingekuja bila dosari. Nikisema Ripoti hii ina dosari ni kwa sababu hivi sasa kama taifa tunataka kuangalia jamii ambazo zimetengwa ili pia tuweze kuzileta katika taasisi za kiserikali. Tukiangalia jamii ya Wabajuni, ni kati ya zile jamii zilizotengwa ama zile tunasema minority ama kwa Kingereza tunasema marginalised . Namfahamu Umra kabisa. Nimejua Umra akiwa mwanamke akitetea harakati za mazingira na mambo ya mabadiliko ya hali ya anga. Pia ameweza kuwa katika shirika linaloitwa Safari Doctor . Nimemjua, hata aliekeza sana na vijana na kina mama katika kujenga mikoko katika sehemu za Pwani, haswa Lamu. Kwa hivyo, nataka nimwambie Mwenyekiti wa Kamati hii aweze kurudia tena mambo haya ya Ripoti, na tuweze kumregesha Umra. Kama mama lazima tusimame na akina mama ambao ni wachache katika zile nyadhifa za kufanya maamuzi. Kwa hivyo, lazima tuangalie tujenge ukenya na tujenge pia zile jamii ambazo zimetengwa. Pia tuweze kuendeleza akina mama. Ukiangalia, wamekuwa watu wanne pale. Tuna Emily na kuna wale wengine. Lakini je, tukiwa na wamama wawili na kina baba wawili, basi tutakuwa na yale tunayoyazungumzia ya thuluthi mbili. Tunaweza kuyafikia tukiwa tutaendelea kwa njia kama hivo. Nataka niseme kuwa Ripoti hii, dosari yake ni hiyo tu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}