GET /api/v0.1/hansard/entries/1222958/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1222958,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222958/?format=api",
    "text_counter": 57,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Mhe. Spika wa Muda. Tumekuwa na hili suala la kutengeneza sehemu hususan za kuzalisha bidhaa za kuenda nchi za ughaibuini kwa muda mrefu. Tumekuwa nalo tangu likiwa linajaribiwa. Nasema “kujaribiwa” kwa sababu ijapokuwa tuko na taasisi mbali mbali za kushugulikia suala la kutengeneza bidhaa kwa minajili ya kupeleka nje, mpaka sasa halijafaulu. Kwa hivyo imefika wakati Mhe. Elachi kuleta hiyo Hoja. Mbali na kumpongeza, tufikirie kwa nini zile taasisi ambazo zipo kwa sasa hazijatimiza lile lengo. Hii inatokana kuanzia sisi tunaotengeneza sheria. Naona hatujatengeneza sheria ambazo zingesaidia kuona kwamba jambo hili linafanyika vizuri. Kwa mfano, kule kwetu Kwale kunachimbwa madini hivi sasa. Nakubaliana na mnenaji aliyetangulia kwamba hili silo suala la nguo peke yake. Ni suala la kuona ni vipi rasilimali zetu, zile ambazo Mwenyezi Mungu ametujalia, zinaweza kusaidia hii nchi, kusaidia serikali kuleta fedha za kigeni, na kusaidia vijana wetu kupata ajira."
}